Man u fan cries that his team has lost

on Sunday 8 December 2013 with 0 comments

Nairobi vibes crazy stories
MAN U POLE!!
Poleni sana poleni, poleni sana Maniyuu,
Mambo si sawa poleni, mnani msimu huu?
Ushindi hampateni, mwakula hasara juu,
Sote kilio pomoni, laanguka jungu kuu.
Tulizoea mabao, kila siku kwenye shoo,
Tumewaita jogoo, hata uliza ukoo,
Sasa nyinyi msi kwao, mbona mwaingia
ndoo,
Sote kilio pomoni, laanguka jungu kuu.
Tunachekwa tazameni, sisi wenu
mashabaki,
Tunaukosa uneni, japo bado twawashiki,
Ewe Muyes jamani, tuondolee hi dhiki,
Sote kilio pomoni, laanguka jungu kuu.
Haya hatujazoea, kupigwa kama watoto,
Nyinyi nyote mnajua, tukija ni tumbojoto,
Sasa timu chekechekea, tunaziona zi moto,
Sote kilio pomoni, jungu kuu laanguka.
Kacha wetu Fagasoni, heri usingeondoka,
Tusingekuwa na soni, za mambo
kuturaruka,
Si njiani si ugani, mambo ni mbuzi kuruka,
Sote kilio pomoni, jungu kuu laanguka.
Nairobi vibes stories

Category:

POST COMMENT

0 Comments:

Post a Comment